Mshambuliaji
Donald Ngoma wa Yanga amerejea mazoezini na matumaini makubwa atacheza mechi ya
Jumatano dhidi ya African Sports.
Katika mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Garanosi mjini Tanga, leo. Kocha Hans van
der Pluijm alionekana kuwa naye karibu akimfundisha mambo kadhaa, hali
inayoonyesha amerejea.
Yanga ilimkosa
Ngoma ambaye alikuwa majeruhi katika mechi yake dhidi ya Mgambo iliyoisha kwa
sare ya bila bao, juzi.
Kurejea kwake
itakuwa ni sehemu ya kufufua matumaini ya kupata pointi zote tatu dhidi ya
African Sports ambao wameishatamba hawana hofu na Ngoma pia Yanga kwa ujumla.







0 COMMENTS:
Post a Comment