Mshambuliaji nyota wa TP Mazembe na Tanzania
Mbwana Ally Samatta ameweka rekodi nyingi mpya baada ya leo kutangazwa kuingia
fainali ya kuwania tuzo za mwanasoka bora Afrika kwa wanaocheza ndani ya bara hili 2015
Samatta ni mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa
Afrika, ameingia na vigogo wengine lakini bado anaweza kuwa na nafasi ya kutwaa
tuzo hiyo.
Fainali au wachezaji waliongia hiyo tatu
bora kwa wanaocheza Afrika ni Baghdad Boundjah (Algeria/ Etoile du
Sahel-Tunisia), Mbwana Ally Samatta (Tanzania/ TP Mazembe-Congo DR), na Robert
Kidiaba (DRC/ TP Mazembe-Congo DR).
Kwa upande wa
walioingia fainali wanaowania tuzo hiyo kwa Afrika hasa wanaocheza nje ya bara
hili ni;
Andre Ayew (Ghana/ Swansea City-England),
Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon/ Burussia Dortmund-Ujerumani) na Yaya Toure
(Ivory Coast/ Manchester City-England).
Kwa sasa Samatta
yuko nchini Japan akiitumikia TP Mazembe katika michuano ya klabu bingwa ya
dunia.








0 COMMENTS:
Post a Comment