Hata timu kubwa au kongwe wakati mwingine zinakuwa na visingizio vinavyoweka kwenye kundi la vichekesho.
Manchester United nao wametoa kali, kwamba joto kali
katika vyumba vya kubadilishia nguo kwenye Uwanja wa Volkswagen lilikuwa ni
tatizo kubwa kwao.
Man United walipigwa wenyeji wao Wolfsburg wa
Ujerumani kwa mabao 3-2 na kung’olewa kwenye mbio za kuwania kucheza Ligi ya Mabingwa
Ulaya.
Man Unitd wanaporomoka hadi kwenda katika michuano ya
Euro kitu ambacho mashabiki wengi wanaona kama si saizi yao.
Taarifa zimeeleza kwamba Kocha wa Man United, Louis
van Gaal na wachezaji wake walilazimika kuomba kuongezwa kwa hali ya hewa ya
baridi wakiwa vyumbani kwani ilikuwa ikiwasumbua sana. Eeh!











0 COMMENTS:
Post a Comment