Mshambuliaji mpya aliyetua nchini
kujiunga na Yanga, Issoufou Boubacar Garba 'Diego' atalazimika kusubiri
hadi Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm ajiridhishe.
Pluijm ameamua kumchukua Diego katika
kikosi cha Yanga kinachokwenda Tanga leo kwa ajili ya mechi mbili za Ligi Kuu
Bara.
Ikiwa Tanga, Yanga itacheza dhidi ya
Mgambo Shooting Jumamosi kabla ya kuivaa African Sports.
Hivyo, Pluijm atatumia muda wa
mazoezi ya timu kuangalia uwezo wa mshambuliaji huyo kutoka Afrika ya Kati.
Yanga imeamua kumuacha Coutinho raia
wa Brazil ili kumpata mshambuliaji mbadala na Diego ni kati ya wanaovizia
nafasi hiyo.








0 COMMENTS:
Post a Comment