Watazamaji wa runinga ya Azam TV wamekumbushwa kula raha kupitia king’amuzi cha Azam TV ambacho kina kila kitu.
Mkuu wa Masoko wa Azam Media, Mgope Kiwanga amesema king’amuzi cha Azam TV kimejitosheleza kwa watazamaji wake na kina mambo mengi ambayo watafurahia wakati wa sikukuu.
“Watazamaji wa king’amuzi cha Azam wana kila sababu ya kufurahia sikukuu kuanzia Maulid, Krismasi na mwaka mpya,” alisema.
“Kuna kila kitu, filamu, tamthiliya, taarifa za habari kwa lugha za Kishwahili, Kingereza na lugha nyingine. Michezo mbalimbali kuanzia nyumbani na sehemu nyingine kote duniani.”
Kwa sass king’amuzi cha Azam TV ndiyo kinachoshika namba moja kwa kupendwa zaidi na Watanzania kutokana na kuwa na mambo mengi ya kuvutia lakini bei zake ni nafuu kuliko ving’amuzi vingine.







0 COMMENTS:
Post a Comment