Mshambuliaji Issoufou
Boubacar Garba 'Diego' tayari ameanza mazoezi na kikosi cha Yanga.
Diego raia wa Niger
ametua nchini jana, leo ameanza mazoezi akiwa na Yanga chini ya Kocha Hans van
der Pluijm.
Katika mazoezi ya Yanga
yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Polisi jijini Dar es Salaam, Diego alipata
nafasi ya kuonyesha vitu kadhaa.
Hata hivyo, Kocha
Pluijm ameamua kumbeba mshambuliaji huyo kwenda naye Tanga ambako atapata
nafasi zaidi ya kumuangalia kabla ya kupitisha uamuzi wa kumsajili au la.
Mshambuliaji huyo
anatumia mguu wa kushoto na anatarajiwa kuchukua nafasi aya Coutinho kama kocha
huyo Mholanzi atamkubali.
Kabla ya kuja nchini,
amewahi kuichezea klabu kongwe ya Tusinia ya Club African na ES Hammam-Sousse
ingawa inaonyesha hakuwa akidumu katika kila klabu hata kwa msimu mmoja tu!
0 COMMENTS:
Post a Comment