December 9, 2015


Yanga na Simba ndiyo wakongwe katika soka la nyumbani na huenda wanapaswa kuwa mfano katika mambo mengi sana.


Lakini mambo yanavyokwenda wamekuwa wakichelewa na kuwa wa mwisho katika mambo mengi sana pia.

Suala la wachezaji kuwa katika mwonekano mzuri wanapokuwa wanasafiri, inaonekana kama hilo litafanyika lazima wavae ‘traksuit’.

Hivi kwani wao hawawezi kuvaa angalau suti na kuwa katika mwonekano bomba kabisa. Mfano angalia picha hiyo ya vijana wawili nyota Watanzania.

Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, hawa wawili wanakipiga katika klabu ya TP Mazembe. Picha hiyo inawaonyesha wakiwa nchini Japan walikokwenda kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia kwa upande wa klabu.

Lazima tukubali, kupitia mengi tunaweza kujifunza kupitia Ulimwengu na Samatta. Vijana wetu, wadogo zetu, ndugu zetu hawa lakini juhudi zao zinafanya watupe somo kubwa na lazima tuziheshimu na kuzithamini.

1 COMMENTS:

  1. Saleh ally hawa simba na yanga wapuuzi wanakalia mipira ya ulaji kufitiniana wao kwa wao vijembe vingi na maneno ya vijembe hata upgeje kelele hawa ni mazuzu tu ebu tzama vijembe vya jery muro na mwenzie haj manara ni upayasi na upuuzivusio jenga mpira kabisa kaka saleh ebu sku moja chukua mda wako utumbue utumbo unaosemwaga na hawa akna jery na manara kabla magufuli hawatumbua. Nakukubaliga sana saleh mpira wetu unabidi utumbuliwe kwanza hata azam wao pia walishaanza siasa uchwara

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic