Kikosi cha
TP Mazembe kipo katika mji wa Osaka, Japan ambako kitacheza mechi zake mbili za
kwanza za Kombe la Dunia.
Mabingwa
hao wa Afrika wamefikia katika hoteli ya Intercontinental ambayo ni moja ya
hoteli bora kati ya hoteli bora kabisa 170 duniani.
Ili
kuonyesha Wajapani wanajua biashara, walichoamua ni kubadilisha baadhi ya rangi
za vyumba vya hoteli hiyo na kutumia nyeusi na nyeupe kwa heshima ya TP
Mazembe.
Meneja wa
TP Mazembe, Frederic Kitenge ameonekana kuridhishwa kabisa na hali ya utulivu
na ubora wa hoteli hiyo ambayo mabingwa hao wakiwemo Watanzania wawili, Mbwana
Samatta na Thomas Ulimwengu, wamefikia hapo.











0 COMMENTS:
Post a Comment