Yanga imeanza kujifariji eti uwezo wa kiungo
mshambuliaji wake mpya, Issofou Boubacar raia wa Niger ni sawa na ule wa nyota
wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi.
Kauli hiyo imekuja baada ya baadhi ya wadau wa
soka nchini kuponda uwezo wa Bobacar anayemudu kucheza winga za kulia na
kushoto pia kiungo cha ushambuliaji kuwa hana jipya kikosini.
Yanga imemsainisha Boubacar mkataba wa mwaka
mmoja katika dakika za mwisho, usajili ambao umeonekana kuwa na shaka huku
ikionekana kuwa mchezaji huyo hakuwa akipata nafasi alipokuwa akicheza
Esperance ya Tunisia.
Katibu Mkuu wa Yanga, Dk. Jonas Tiboroha
amesema kuwa: “Nashangaa baadhi ya watu wanaomponda Boubacar,
kukaa benchi ni kitu kingine lakini mimi naamini ana uwezo kama wa Okwi tu.”
“Ukimtazama vizuri utaona Boubacar ana kasi na
mbinu nyingi kama zile za Okwi, yaani huyu anafanana sana na Okwi hakuna ubishi
katika hilo na watu watamuona siku akicheza.”
Alisema katika soka kuna vitu vingi na ndiyo
maana Boubacar hakupata nafasi Esperance lakini anaamini atafanya vizuri akiwa
Yanga wakati huu.







0 COMMENTS:
Post a Comment