December 12, 2015


Kikosi cha Simba kinashuka dimbani Taifa leo kuwavaa Azam FC katika Ligi Kuu Bara, lakini kama mambo yakienda vizuri straika wake Paul Kiongera ataichezea kwa mara nyingine timu hiyo, ila kuna kitu kimemsononesha.

Kiongera wakati anakuja kuendelea na mkataba wake wa kuichezea Simba, alipanga aje avae jezi namba tano lakini ghafla ndoto zake zimeyeyuka na sasa atacheza huku akiwa amevaa jezi namba 29. Wakati akiwa Simba alikuwa akitumia jezi namba 12 ambayo hata hivyo haikuwa chaguo lake namba moja.

Aliyemnyima jezi hiyo Kiongera ni Hamis Kiiza raia wa Uganda ambaye sasa anaivaa jezi namba tano na hana mpango wa kuachana nayo, ndiyo maana straika huyo inabidi avae namba 29.

“Nilipokuwa nakuja Simba nilitaka kuvaa namba tano, lakini hapa nimekuta inavaliwa na Kiiza sasa sina jinsi na inanibidi nivae namba 29 japokuwa halikuwa chaguo langu,” alisema Kiongera.

Kiongera aliyewahi kucheza Gor Mahia ya Kenya, amerejeshwa katika kikosi cha Simba akitokea KCB ya Kenya pia ambako alikuwa akicheza kwa mkopo akitokea kwa Wekundu wa Msimbazi.
Katika mechi ya leo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam, Kiongera anaweza kucheza kama mambo yakienda vizuri.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic