December 12, 2015


Jamaa haishi maneno, Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema hatishiki hata kidogo na uwezo wa kufunga alionao straika Elias Maguri wa Stand United, kwani lazima atazuiwa leo.

Leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Kamabarage Shinyanga, Mwadui itacheza na Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali kwa timu hizo za mkoa huo.

Maguri kwa sasa ndiye mshambuliaji hatari zaidi katika ligi kuu akiwa amefunga mabao tisa na kuwapiku nyota kama Donald Ngoma wa Yanga na Hamis Kiiza wa Simba wenye mabao nane kila mmoja.

Julio amesema kuwa; “Najua Maguri ni mchezaji mzuri, lakini hawezi kufanya kitu mbele ya kikosi changu kilichosheheni nyota kibao wenye uzoefu.

“Siyo kwamba naibeza Stand United moja kwa moja, ila nasema ukweli kwamba tupo vizuri kucheza nao na mashabiki wetu wategemee jambo zuri kutoka kwetu.”


Katika msimamo wa ligi kuu, Stand United ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 19, wakati Mwadui ipo nafasi ya saba ikiwa na pointi 15.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic