| AZAM FC |
Kocha wa Simba, Dylan Kerr amesema anatamani leo Azam FC imchezeshe kipa Ivo Mapunda, ili aone kama alikosea au yupo sahihi kuondoka katika kikosi chake.
Mapunda amejiunga na Azam akitokea Simba ambako amemaliza mkataba wake, hivyo Kerr anataka kuona vipi bado ana vitu au ameshaisha lakini zuri zaidi ni kwamba wanamjua, hivyo atawarahisishia ushindi.
Kerr amesema: “Nataka kumuona Ivo yupoje kwa sasa, natamani sana achezeshwe, lakini nikuambie kitu, sisi tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunaifunga Azam.
| KERR |
“Kwanza najua kuwa mechi yetu hii ya leo itakuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na kila timu kujiandaa kikamilifu kuibuka na ushindi dhidi ya mwenzake.
“Natamani wampange Ivo kwani tunamjua na itakuwa rahisi kwetu kupata ushindi.”
Kwa upande wake Kocha wa Azam, Stewart Hall, alipotakiwa kuzungumzia mchezo huo, muda mwingi alikuwa akicheka na kujibu kirahisi kwamba tutaona kitakachotokea.
Mchezo huu wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ndiyo unaotarajiwa kutoa picha kwa Azam kwani ikishinda itafikisha pointi 28 na kuzidi kujichimbia kileleni kwani inayofuatia ina pointi 23 na hata ikiifunga Mgambo JKT leo itafikisha pointi 26 tu.







0 COMMENTS:
Post a Comment