| HENRY (KULIA) WAKATI AKIWA SIMBA KABLA YA KUHAMIA MTIBWA |
Kiungo wa zamani wa Simba, Henry Joseph, amepewa jukumu la kuiongoza Mtibwa Sugar mbele ya Mbeya City katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Joseph amepewa jukumu la kucheza nafasi ya kiungo ya Shaaban Nditi, pia atakuwa nahodha kuchukua nafasi ya nyota huyo ambaye ni majeruhi sasa.
Kazi ya Joseph itakuwa ni kuhakikisha Mtibwa inaifunga Mbeya City yenye nyota kibao akiwemo kipa Juma Kaseja na kiungo Haruna Moshi ‘Boban’.
Mtibwa ina pointi 22 katika nafasi ya tatu wakati Mbeya City ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi tisa tu.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Ofisa Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru, alisema: “Henry Joseph amepewa jukumu la kuziba pengo la nahodha Shaaban Nditi ambaye kutokana na kuwa majeruhi, ataukosa mchezo huo.”
“Tunataka tushinde mchezo huu, ndiyo maana Joseph amepewa kazi za Nditi na tunaamini ataweza kufanya hivyo bila tatizo lolote.”







0 COMMENTS:
Post a Comment