MPIRA UMEKWISHAAA
Dk 90+3 Simba inapata kona mfululizo, lakini wanashindwa kuzitumia
Dk 90+2 Everisti Benard anaifungia Toto bao la kusawazisha baada ya beki Hassan Isihaka kushindwa kuruka juu na kupiga kichwa, mpira ukamkuta mfungaji
Dk 88, Everist Benard naye anapata nafasi nzuri ya kupiga kichwa lakini anapaisha juu kabisa
Dk 87, Jaffar Mohammed anabaki yeye na kipa wa Simba baada ya Juuko kuanguka, lakini anapiga pembeni kabisa na mabeki wa Simba wanaokoa
Dk 84 mpira umesimama, Khatibu, nahodha wa Toto yuko chini anatibiwa baada ya kuumia mguu wakati akishuka chini aliporuka kuwania mpira wa kichwa na Lyanga
Dk 81 Japhet Makaranga anapiga krosi safi kabisa, lakini mabeki wa Simba wanaokoa
Dk 76 Lyanga anakwenda chini, analala pale chini. Ni baada ya Hassan Hatibu kumpiga na mkono wakati wakigombea mpira. Anatolewa nje kwenda kutibiwa
Dk 63 Lyanga anamtoka Carlos na kupiga mpira lakini kipa anapangua na mabeki wanaondosha
DK 62, Kiongera akiwa eneo la 12 la lango la Toto anapokea krosi nzuri ya Kessy lakini anapiga shuti kuuubwaaa
Dk 59 Kiongera anaingia na kugusa nyasi za CCM Kirumba
Dk 57, Japhet Vedastus Makaranga anawatoka mabeki wawili wa Simba, anapiga krosi inaaokolewa na kuwa kona. Anaichonga mwenyewe lakini Agban anafanya kazi ya ziada
DK 55, Ajibu anapiga mkwaju hatari kabisa, kipa anadaka na kuutema unamkuta Kiiza, mwamuzi anasema ni offside
Dk 47, Madenge au Sheva Go anaingia na kupiga shuti kali sana, mpira unagonga mwamba na kumrudia Agbani ambaye anaudaka haraka
MAPUMZIKO
DK 42 Mkude anajitahidi kutawala safu ya kiungo lakini ladha ya soka imepotea
Dk 37 hadi 40, zaidi mpira unachezwa katikati lakini muda mwingi wachezaji wanaanguka tu kutokana na utelezi
Dk 36, pasi nzuri ya Madenge, Salimini Hozza anajaribu shuti lakini linaonekana ni laini kwa kipa Agbani wa Simba
Dk 31, Kiiza anatoa pasi ya kisigino kwa Ndemla ambaye anapiga shuti kali lakini 'halina macho'
Dk 29, Lyanga anaingia vizuri baada ya kuiwahi pasi ndefu, anajaribu kumtafuka Kiiza lakini krosi yake inawahiwa na kipa
Dk 24, Kiiza anaumizwa hapa, daktari wa Simba anaingia na kumtoa nje na sasa anapatiwa matibabu
GOOOOOOO Dk 22, Lyanga anawafunga bao safi kabisa nje ya 18, baada ya kuona kipa ametoka anapiga mpira wa juu unaaa wavuni, Simba moja.
Dk 19, Simba inaendelea kufika mara nyingi zaidi katika lango la Toto lakini ugumu unaonekana kwa kila upande kutokana na madimbwi uwanjani
Dk 15 Lyanga anaangushwa, mwamuzi anasema faulo na inachongwa na Ndemla, anapiga vizuri lakini kipa wa toto anafanya kazi nzuri kuokoa na kuwa kona.
Dk 14, Chukwu anaingia na kupiga shuti kali, linatoka pembeni kidogo sana mwa lango la Simba
Dk 11, Kiiza anamtulizia Ndemla anapiga shuti kali linaokolewa na kuwa kona. Inachongwa na Ajib lakini madhambi yanafanyika
Dk 9, mpira bado unaonekana kutokuwa na radha nzuri kwani mara kadhaa mpira unanasa kwenye madimbwi ya maji hapa Kirumba
Dk 6, Miraja Athuman Madenge anajaribu kumtoka Juuko lakini anamuangusha na mwamuzi anaamuru ipigwe faulo. Si mbali na lango la Simba lakini inakuwa haina mashara
Dk 3 Kessy anaingia vizuri na kumpa Mkude pasi nzuri lakini anateleza na kuanguka
Mechi imeanza lakini inaonekana itakuwa mechi ngumu iliyokosa ufundi kwa kuwa uwanja wa Kirumba umejaa maji chapachapa na wachezaji wanasumbuka hata kukokota mpira







0 COMMENTS:
Post a Comment