MPIRA UMEKWISHAAAA
Dk 90 Katura aliyeingia kuchukua nafasi ya Kiemba katika dakika ya 68, analambwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kiwiko kwa makusudi Tambwe
Dk 87, Msuva anapata nafasi nzuri lakini anafumua shuti laki juuuu
SUB Dk 86 Pato Ngonyani anaingia kuchukua nafasi ya Yondani aliyeumia
KADI 84 Duna wa Stand analambwa kadi ya njano kwa kumkanyaga Yondani
Dk 82, Matheo anaingia vizuri baada ya pasi ya Tambwe kumfikia lakini Chollo anaokoa na kuwa kona. Yanga wanachonga kona lakini inaonekana haina madhara
SUB Dk 79 Yanga wanamtoa Kaseke, nafasi yake inachukuliwa na Gofrey MWashiuya
SUB Dk 78 Selemani Mrisho anaingia kuchukua nafasi ya Abuu Ubwa upande wa Stand United
Dk 75 Said Khamis anapiga shuti kali lakini linagonga mwamba na kuokolewa
SUB Dk 74 anatoka Ngoma anaingia Anthony Matteo
SUB Dk 73 anatoka Maguri nafasi yake inachukuliwa na Said Khamisi
Dk 70 hadi 73, mpira unachezwa katikati zaidi lakini Yanga wanaonekana kuridhika na mabao hayo manne hivyo hawana presha. Lakini Stand hawaonyeshi tena hamu ya kutaka kusawazisha
SUB Dk 68 Stand wanamtoa Kiemba anaingia Jeremiah Katula
Dk 64 Kamusoko anaifungia Yanga bao safi kabisa ambalo linakuwa la nne katika mechi hii
Dk 55 hadi 60, bado hakuna mashambulizi makali, Yanga wanaonekana kucheza kwa umakini mkubwa wakijaribu kutafuta bao la nne huku Stand wakitaka kusawazisha
Dk 50 hadi 51, Stand wanaendelea kupoteza mpira kila wanapokaribia lango la Yanga hali inayofanya kutokuwa na mashambulizi makali yanayipelekwa upande wa lango la YAnga
Dk 46 kipindi cha pili kinaanza kwa Stand kushambulia lakini hata hivyo inaoenekana Maguri na wenzake hawako makini na wamekuwa wakipoteza mipira kwa ulaini.
HALF TIME
GOOOOOO Dk 45, Tambwe tena anautegua mtego wa mabeki wa Stand na kufunga bao la tatu kwa shuti kali sana baada ya kupokea pasi nzuri ya Ngoma. Hat trick na bao lake la nane
Dk 42, Chanongo anapiga shuti kali, linagonga mwamba na kuokolewa
Dk 40, Juma Abdul analala na kuokoa mpira unakuwa kona, Stand wanaichonga vizuri na Chanongo anapiga shuti kali lakini Dida anadaka kwa uzuri kabisa
GOOOOOOO Dk 36 krosi nzuri ya Juma Abdul, Amissi Tambwe anaruka juu na kufunga bao safi la kichwa. Hili ni bao la sita kwake msimu huu
Dk 31 hadi 36, Kamusoko na Makapu wanabadilika na kutawala sana kiungo
Dk 29 hadi 31, Kiemba anaonekana kutawala vizuri katika kiungo huku akimpa wakati mgumu Makapu
Dk 26, Maguri anatoa pasi nzuri kabisa kwa Kiemba ambaye anazongwa na mabeki wa Yanga anashindwa kutulia na kuutoa nje, goal kick
KADI Dk 21 Said Juma Makapu wa Yanga naye analambwa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi MAsawe
KADI Dk 20 Jacob Massawe anakuwa wa kwanza kuoga kadi ya njano katika mechi hii baada ya kumuangusha Tambwe
GOOOOOOO Dk 19 Tambwe anaifungia Yanga bao safi kabisa baada ya mabeki wa Stand kuzubaa
Dk 11, Chanongo anaingia vizuri na kupiga shuti kali lakini anashindwa kulenga lango
Dk 7, Juma Abdul anaingiza krosi safi kabisa lakini Kamusoko anashindwa kuiwahi, inatoka nje
Dk 4, Stand wanakuwa wa kwanza kufanya shambulizi, krosi nzuri ya Chanongo, Haji Mwinyi anaokoa na kuwa kona. Inachongwa lakini Dida anaokoa na kuwa kona tena, inachongwa Yanga wanaokoa
Mechi imeanza na kila timu inaonekana kumsoma mpinzani wake kwa kupiga pasi za taratibu katikati ya uwanja kufanya buil up.








0 COMMENTS:
Post a Comment