December 12, 2015



Dk +2
KADI Dk 90 kipa Vicent Agban analambwa kadi ya njano kwa kumvuta mchezaji wa Azam FC wakati akijaribu kufunga akiwa amemtoka yeye
Dk 89, Simba wanajaribu kugongeana lakini sasa bado wanapoteza mipira mingi katikati

Dk 86, Kapombe anashindwa kufunga akiwa mbele ya lango la Simba
SUB Dk 85 Simba wanamtoa Emiry anaingia Hassan Kessy
SUB Dk 82 Simba wanamtoa Banda anaingia Peter Mwalyanzi-Azam FC wanamtoa Kipre anaingia Mudathir Yahya 

Dk 81, Simba wanaonekana kupoteza umakini katika ulinzi kadiri muda unavyosonga
Dk 80, Kipre anamhadaa Emiry, anapiga shuti kali lakini linagonga mwamba na kumrudia kipa

Dk 75, Bolou anaingia na kupiga shuti kali, linatoka nje kidogo. Ni baada ya beki ya Simba kufanya uzembe kama ule wakati wa bao la pili, kupoteza mpira halafu wakazembea kukaba

GOOOOOOO Dk 72 Bocco anaifungia Azam bao la pili baada ya uzembe wa kupitiliza wa mabeki wa Simaba
SUB Dk 71 Azam FC wanamtoa Sure Boy, nafasi yake inashukuliwa na Didier Kavumbagu
SUB Dk 70, Simba inamuingiza Hamisi Kiiza kuchukua nafasi ya Lyanga

GOOOOOO Dk 68 Ajib anampindua Said Morad, anaingia na kufunga kwa ufundi kabisa wakati Wawa na Aishi wakidhani anapiga krosi
Dk 62 hadi 66, Simba wanatawala zaidi wakipiga pasi za uhakika na kusababisha mashabiki wao kushangilia kwa nguvuDk 61, Ajib anamchambua Kapombe, yeye na kipa sasa, anashindwa kulenga lango. Ilikuwa hatari sana kwa Azam FC

Dk 57 hadi 59 Simba bado wanaonekana kupata Dk 59, Lyanga anapiga shuti safi kabisa baada ya pasi nzuri ya Ajib, lakini mpira unapita juu kidog
nafasi kadhaa lakini Azam Fc ni kama wanaosubiri kitu
Dk 54, Lyanga anapata pasi nzuri kutoka kwa Ajib, lakini Aishi anatoka na kuokoa, Lyanga anautoa mpira nje

Dk 49, Lyanga anaonekana kuendelea kuwa msumbufu ingawa kwenye safu ya ulinzi ya Azam inayoongozwa na Wawa kunaonekana kuwa na nidhamu
Dk 46 hadi 49, Simba wanaonekana kuwa wasumbusu zaidi wakicheza m,pira wa kasi hali inayoonekana kuwachanganya Azam FC
MAPUNZIKO
KADI (DK 45 Emiry Nimubona, analambwa kadi ya njano kwa kuvua jezi kabla ya kutoka uwanjani)
Dk 45, Ajibu anagongeana vizuri na Lyanga lakini Aishi anaingilia na kuokoa vizuri
Dk 44 Lyanga tena anaingia katika eneo la hatari lakini anapaisha
Dk 42 Lyanga anapata pasi nzuri kutoka kwa mchezaji wa Azam Fc aliyejichanganya, anaingia na kupiga vizuri lakini unapita nje
Dk 38, Simba wanapoteza nafasi nzuri kabisa, Kiongera yeye na kipa, anapiga lakini Aishi anaokoa vizuri kabisa

Dk 37, Tchetche anageuna ndani ya eneo la hatari la Simba, anatoa pasi safi kwa Bocco lakini ni offside

KADI Dk 35 mwamuzi Erick kutoka Arusha anatoa kadi ya njano kwa Kipre Tchetche kwa kujiangusha ndani ya eneo la 18
Dk 30 hadi 32, inaonekana timu zote zaidi zinacheza katika ya uwanja
Dk 29 Lyanga tena anamtoka Moradi na kupiga shuti kali, kipa anaokoa unatoka lakini mwamuzi hakuona, inakuwa goal kick
Dk 28, Lyanga anapiga kichwa hatari kabisa lakini Manula anafanya kazi ya ziada, anaokoa, mpira unagonga mwamba na kuwa kona, lakini haina mashara

Dk 27 Bocco anapata pasi nzuri ya Sure Boy anaingia na kupiga shuti linaokolewa na Isihaka na kuwa kona, lakini haina mashara

KADI Dk 26, Ajibu analambwa kadi ya njano kwa kuvua shati wakati anashangilia

GOOOO Dk 25 Ibrahim Ajibu anamtoka Moladi na kufunga bao safi ilikuwa ni baada ya kupokea pasi nzuri ya Ndemla
Dk 23, Lyanga tena anaingia na kupiga shuti kali lakini linadakwa kwa ulaini
Dk 18, Mkude anatoa pasi nzuri kwa Mohammed Husseein anapiga krosi nzuri lakini mpira unakosa mmaliziaji
Dk 13 Danny Lyanga anaingia vizuri na kupiga shuti lakini mpira unatoka nje
Dk 6 hadi 8, Simba wanaonekana kushambulia zaidi huku Azam wakilinda na kuituliza presha
Bao la kwanza la Azam FC limefungwa katika dakika ya kwanza na mshambuliaji na nahodha wa timu hiyo John Bocco.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic