December 12, 2015


Pengo la mshambuliaji Donald Ngoma limeonekana wakati Yanga ikitoka sare ya bila kufungana dhidi ya wenyeji wake Mgambo Shooting.

Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, safu ya ushambuliaji ya Yanga ilionekana kutokuwa na meno kutokana na kumkosa Mzimbabwe Ngoma ambaye ni majeruhi.

Mgambo walianza kuitoa Yanga mchezoni kwa kuichezea kindava hasa katika kipindi cha kwanza.

Baada ya hapo, Mgambo walikuwa wakishambulia kwa kasi na kukaba kwa nguvu hivyo kuichanganya Yanga.

Kama wangekuwa makini,basi Mgambo wangeshinda mechi hiyo katika kipindi cha pili baada ya kutawala sehemu ya kiungo na Yanga kuonekana kuishiwa nguvu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic