December 22, 2015

MACHUPPA...

Mshambuliaji nyota wa zamani wa Simba, Athumani Machuppa amezua mjadala wa Diamond na Ali Kiba.

Mjadala huo umezuka kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook baada ya kusema Diamond ni msanii mkali.

Post hiyo ya Machuppa kuonyesha anamkubali Diamond ilizua mjadala kwa wachangiaji.

DIAMOND

Wako walianza kumsifia kuungana na Machuppa ambaye sasa anaishi nchini Sweden, lakini wengine walionyesha kupinga wazi wakisema hana lolote ni wa kawaida.

Wengine walienda mbali zaidi baada ya kusema Diamond “anasubiri” kwa mtoto wa Kariakoo wakiwa wanamaanisha Ali Kiba ambaye anaonekana ndiye mpinzani wa Diamond.

ALI KIBA
Hata hivyo Machuppa alionekana kumaliza kiu yake ya kusifia alichokuwa anakiamini na kuamua kukaa kimya huku wengine wakiendelea kubishana.


Diamond na Ali Kiba wamekuwa na upinzani mkubwa kupitia mashabiki wao wa muziki. Kila mmoja akiamini msanii mmoja ni mkali kuliko mwingine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic