December 22, 2015

DK TIBOROHA AKIWA NA JERRY MURO
Uongozi wa Yanga umekubali kwamba msemaji wake, Jerry Muro alikosea kuzungumza maneno yaliyolenga kuwasharau watu wa kabila la Wazaramo.

Lakini ukaomba radhi wote waliokwaza na maneno makali ya Muro ambaye alizungumza wakati akimshambulia Msemaji wa Simba, Haji Manara.

Katibu Mkuu, Dk Jonas Tiboroha amesema Muro alikosea na anapaswa kusamehewa lakini uongozi wa Yanga unalifanyia kazi.

“Wazaramo ni asili ya Yanga, hivyo hatuwezi kukaa kimya mtu akionyesha dharau kwao. Ninaamini bwana Muro alisema hayo akiwa na mihemko.

“Jambo zuri kuzungumza na kusikiliza unachosema, tuwaombe radhi wote waliokwazika.

“Msisitizo ni jambo zuri kuheshimiana katika masuala ya mpira kuliko kudharauliana. Tunaendelea kufanya uchunguzi na mwisho tutaeleza kuhusiana na msimamo wetu.
“Iwapo tutabaini kwamba Muro alifanya hivyo kwa kukusudia, basi tutachukua hatua kali,” alisema Dk Tiboroha.

Muro alisema maneno yaliyoashiria kashfa kwa kabila la Wazaramo wakati akimshambulia Manara ambaye amezaliwa na kukulia Kariakoo.


Hii ni mara ya kwanza uongozi wa Yanga kuomba radhi, lakini tayari mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga, Mohammed Bhinda ambaye pia ni Mzaramo alikuwa wa kwanza kuomba radhi ingawa bado Muro hajazungumza lolote kuhusiana na suala hilo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic