December 23, 2015


Mafanikio makubwa kwa Leicester City katika Premier League hadi kufikia Krismasi, kumeongeza kwa kiasi kikubwa soko la wachezaji Riyad Mahrez na Jamie Vardy.

Washambuliaji hao wanaoonekana kuwa na soko kubwa zaidi kabla hata dirisha dogo la usajili halijafunguliwa Januari, mwakani.

Wawili hao wamekuwa moto wa kuotea mbali na sasa Leicester City inaongoza Ligi Kuu England ikifuatiwa na Arsenal na Man City.

Mahrez raia wa Algeria, sasa amefikia hadi pauni milioni 25 ikiwa ndiyo thamani yake, anafuatiwa na Vardy anayeongoza kwa kufunga sasa, yeye ni pauni milioni 20.


Wengine ni mshambuliaji wa Watford, Odion Oghalo pauni milioni 15, Yanick Bolasie wa Crystal Palace pauni milioni 18 na Dimitri Payet wa West Ham, naye pauni milioni 18.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic