Serikali imelazimika kuingilia kati na kuutatua mgogoro uliokuwepo ndani ya timu ya Stand United.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alisema kuwa wizara yake ilikaa kikao kuangalia kwa kina mgogoro huo na kubaini unasababishwa na kamati iliyoundwa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Lufunga ambayo inashinikiza kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wapya.
Alisema kuwa baada ya kubaini hilo wakaona njia ya kuondoa mgogoro huo ni kuitimua kamati hiyo hiyvyo ameitaka itoke mara moja na kuiacha timu hiyo kuwa chini ya uongozi uliopo sasa chini ya Mwenyekiti wake Amani Vicent.
“Tulipongia kazini tulisema moja ya migorogo mikubwa katika michezo ipo katika klabu za mpira lakini ukiangalia mgogoro huu kiundani ni wa kimaslahi kwa sababu Stand United ilipoanzishwa ilikuwa inafadhiliwa na wale wapiga debe ambao walikuwa wakichangisha wenyewe kuendesha timu yao na hakukuwa na migogoro. Imefanya vizuri wakaingia watu wa Acacia kuidhamini timu hiyo.
“Malalamiko makubwa ni kwamba kuna timu imeundwa na mkuu wa mkoa ambayo inajaribu ku-manage fedha za udhamini sasa ukiliangalia hilo suala linaweza kuwa na nia njema lakini inawezekana kwa namna linavyoendeshwa limeminya uhuru wa Stand kujiendesha wenyewe.
"Tulichokubaliana sisi wizara tumeingilia kati kuhakikisha uhuru wa timu kuendesha mambo yao wenyewe kwa sababu wanakatiba na tarabu zao ili mradi wazizangatie hizo.
“Uongozi unarudishiwa mamlaka yake na kusimamia mambo yao, lakini wakati huo huo mdhamini ahakikishe pesa yake inatumika vizuri ndani ya klabu na uongozi uhakikishe wanaajiri wataalamu wazuri wasimamie fedha watakazopewa.
"Tunaamini tukiufikisha hapo utakuwa umekwisha kwa sababu tatizo ni nani atasimamia fedha hizo kutokana na waliosaini mkataba huo ni watu wa Stand na mdhamini Acacia.
“Sisi kama wizara tuliochokiamua ni kuwa mkuu wa mkoa na watu wake wakae pembeni watu wa Stand waweze kufanya mambo yao wenyewe kwa mujibu wa katiba yao na kama serikali tunaitaka TFF ihakikishe mambo ndani ya klabu hii yanakwenda vizuri,” alisema Nape.








0 COMMENTS:
Post a Comment