Mbeya City imeamua kuchukua pointi tatu katika mchezo wake wa leo Jumamosi dhidi ya Yanga kwa kuwasili Dar es Salaam saa chache kabla ya mchezo huo.
Ikishatua kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Mbeya City itapumzika kidogo katika moja ya hoteli jijini kisha itakwenda Uwanja wa Taifa, kucheza na Yanga mechi ya Ligi Kuu Bara.
Mbeya City yenye wakongwe kadhaa wa ligi kuu wakiwemo Juma Kaseja na Haruna Moshi ‘Boban’, imefanya hivyo ili kutotoa mianya ya kupoteza mchezo huo kwa vitendo vya nje ya uwanja.
Kocha wa Mbeya City, Meja Mstaafu, Abdul Mingange aliliambia Championi Jumamosi kuwa; “Tumeamua kuja siku ya mechi kutokana na kutaka kukwepa hujuma ambazo zinaweza kujitokeza kabla ya kuvaana na wapinzani wetu, tutatua huko saa chache kabla ya mechi.
“Siye tunataka pointi tatu tu, wala hakuna jambo lingine ndiyo viongozi wanaingia gharama kama hizi. Ujue Yanga ipo vizuri kwa sasa kwa hiyo ukicheza nayo unatakiwa kuwa na maandalizi kabambe na siyo lelemama vinginevyo unaweza kupata aibu, sisi tumepanga kushinda.”
0 COMMENTS:
Post a Comment