December 26, 2015


Ukiamua unaweza lakini lazima uwe umeshinikizwa na kitu fulani ili kufikia kilele cha mafanikio, kwani Uhuru Selemani sasa anafanya mazoezi kwa muda wa saa nane kwa siku huko Afrika Kusini.

Uhuru aliyewahi kucheza Coastal Union, Simba na Azam FC sasa anachezea Royal Eagles inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Afrika Kusini lakini analazimika kufanya mazoezi zaidi ili kupata nafasi fisrt eleven.

Uhuru ambaye yupo nchini kwa mapumziko, alisema maisha anayoishi Afrika Kusini tofauti na alivyokuwa hapa kwani analazimika kufanya mazoezi kwa saa zisizopungua nane kwa siku.

“Baada ya kufika kule nilikuta maisha tofauti ya soka na hapa nyumbani, wachezaji wote wapo ‘siriazi’ na kazi yao, na mimi nikaamua kubadilika ili niendane na kasi yao.

“Zamani nilikuwa nikifanya mazoezi kwa saa mbili siku imeisha, lakini kwa sasa natumia saa saba mpaka nane kufanya mazoezi, kwa kweli mimi mwenyewe najiona nimebadilika tena sana, kwa sasa naona soka linalipa tofauti na zamani,” alisema Uhuru aliyeibukia katika soka kutoka Ukwamani FC ya Kawe jijini Dar es Salaam.


“Bila kufanya mazoezi ya nguvu ni ngumu kupata nafasi kikosi cha kwanza, hivyo ni lazima upambane sana mazoezini.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic