December 30, 2015


Wakati uongozi wa Simba chini ya Rais Evans Aveva, ukionesha dalili za kukubaliana na ombi la bilionea, Mohammed Dewji ‘MO’ kuichukua klabu hiyo kwa ununuzi wa hisa, bodi ya udhamini imekuja juu na kupinga hilo.

MO ameweka bayana nia yake ya kuwekeza bilioni 20, kwa ajili ya kurejesha hadhi ya Simba ikiwa haijashiriki michuano ya kimataifa miaka minne sasa.

Aveva alikiri kuwepo na mpango wa MO, lakini akasema kuwa suala hilo linahitaji mchakato mzito mpaka kumfikia maamuzi ya kumpa mamlaka tajiri huyo.

Alisema mojawapo na hatua ni kujadili kwa kina thamani ya timu kisha kulifikisha kwa bodi ya wadhamini kabla ya kuliacha mikononi mwa wanachama katika mkutano mkuu ili kuridhia uwezekano wa kumuuzia hisa za umiliki wa timu.

Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini, Mzee Hamisi Kilomoni, ametoa rai mapema kuwa mpango wa kuiachia timu hiyo kutoka mikononi mwa wananchi hauwezekani kwa hoja yoyote ile.

“Kwanza tangu Aveva aingie madarakani sijawahi kumuona na hajawahi kuonana na kiongozi yeyote wa bodi ya udhamini…MO yeye namsikia tu kwenye vyombo vya habari.

“Hatuko tayari kuiachia timu kwa vyovyote itakavyokuwa, hatuko tayari kuachia timu iwe mikononi mwa mtu mmoja kwa ushawishi wa milioni ngapi…kumbuka hawa wanakuja na kuondoka, sisi tuko palepale na sisi ndiyo wenye hati ya kufanya hivyo (kuidhinisha).

“Siafiki uwekezaji unaozungumzwa, si sahihi  na haujafuata misingi sahihi, vinginevyo tutaitelekeza timu kwa ushawishi wa bilioni 20 za mtu,” alisema mchezaji huyo mwasisi.


Wakati wengi wakiunga mkono adhima ya MO, kwani timu haina cha kujivunia miaka 80 sasa licha ya kuwa chini ya miliki ya wanachama, Mzee Kilomoni alifunguka: “Siyo kweli tuliingia Simba haina jengo, leo hii ina majengo mangapi, uwanja upo lakini wa kulaumiwa ni viongozi wanaongia madarakani mara kwa mara wanashindwa kuuendeleza siyo kweli kwamba timu haina kitu.”

5 COMMENTS:

  1. Haya ndio aina nyingine ya majipu ya kutumbuliwa. Tuko 2015 lkn mzee tunayemheshim anatka tubaki na maisha ya 1945. Mpira wa sasa ni ushindani wa nje kabla ya ushindani wa uwanjani. Ushinde katika soko la usajili na huduma bora kwa timu ndipo utaposhinda kikombe na mafanikio ya uwanjani. Wazee hawa wanahitaji kuelimishwa.

    ReplyDelete
  2. Wazee kama hawa wanadhani wanaipenda klabu lakini ndo wanaimaliza. Achukue mfano wa klabu za nje. Zinamilikiwa na watu lakini bado zina washabiki tena wenye nguvu tu. Mpira ni biashara siku hizi na nguvu ya fedha ndo inakupa uwezo wa kupambana uwanjani. Ona mfano wa Azam, jiulize ingekuwa na washabiki wengi kama wa Simba na Yanga si ingekuwa inachukua ubingwa tu kila siku. Muhimu ni kuzingatia mambo muhimu kabla ya kuuza hisa. Ila naamini timu ikiendeshwa kibiashara itakuwa na mafanikio zaidi, pia na hadhi. Ni aibu klabu kubwa na kongwe kama simba eti inakodi uwanja wa mazoezi. Kwa kweli ni aibu hata kujivunia kuwa klabu yetu ina kitu chochote. Hilo jengo la msimbazi wa si kitu. Klabu kama Mazembe, ina uwanja wake na ndege, Azam wana Mabasi na viwanja viwili, hilo nalo hatuoni...!!

    ReplyDelete
  3. Anazeeka vibaya huyo. Atakua anataka asilima 10
    Haoni timu inavyoshindwa kusajili kutokana na timu haina pesa. Timu.ingekuwa na pesa tunhemshidwa mavugo. Wachezaji tulionao ni wabei rahisi lasivyo ameonekana hafai katika timu flani. Hivi kweli simba ni wakupewa mchezaji kwa mkopo tena kutokea Azam? Nahizi anamawazo mgando haingizi jambo jipya

    ReplyDelete
  4. Hawa wazee mbona wanatia DOA kitumbua? Au kisa wamekua mashabik was simba KWA miaka nying. Ila atambua kila mshabik ana haki ndan simba atakama amezaliwa Jana..wasitumie uzee wao ndani ya simba kutuletea mambo ya kizaman..wanacho taka watu Ni soka...la maemdelo..na watu kama hawafai kabis kwnye maendelo ya soka... Wanarusldisha soka nyuma..tff iwaangalie sana

    ReplyDelete
  5. Na unaazi wa kuipenda timu mpak kutoitakia maendelo ndo kitu tusicho kipenda kabisa..nafikir katiba ifanyiw markebisho ili tuvifunge midomo.HV vizee club isongE mbele...tunavinyamazish kimy kimy.. Kwan unafkir vinajua at a kusom?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic