December 19, 2015


Mshambuliaji mpya wa Yanga, Paul Nonga, kidogo tu ameikosa rekodi ambayo ingekuwa mpya katika Ligi Kuu Bara ambayo alipaswa kuiweka leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Nonga aliichezea Mwadui FC katika mechi iliyopita na kufunga bao moja wakati iizamishs Satand Unite kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Baada ya mechi hiyo alisajiliwa Yanga ambayo inacheza na Stand United leo kwenye Uwanja wa Taifa na kama Nonga angecheza, basi angeweka rekodi ya kucheza dhidi ya Stand United mara mbili ndani ya wiki moja, katika mzunguko mmoja wa ligi.

Bahati mbaya, Nonga hataweka rekodi hiyo kwa kuwa anaondoka kurejea Mwadui Shinyanga kukamilisha masuala yake ya kuhamisha vitu na familia kabla ya kurejea na kuanza kazi Yanga.

Katika mchezo wake wa mwisho akiichezea Mwadui FC, Nonga alifunga bao moja lililoiwezesha timu hiyo kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stand United. Bao lingine lilifungwa na Fabian Gwanse.

Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm amesema Nonga ameomba ruhusa kwa uongozi kwenda kwao kubeba mizigo na kumalizia mambo mengine ili ahamie rasmi Dar es Salaam.

“Nonga ameomba ruhusa hivyo hatocheza dhidi ya Stand, ameenda kwao kumaliza mambo yake na atarejea Dar es Salaam, Jumapili (kesho) ili Jumatatu aanze na wenzake,” alisema Pluijm raia wa Uholanzi. 


Ujio wa Nonga katika kikosi cha Yanga umeongeza idadi ya washambuliaji na kufikia watano, wengine wakiwa ni Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Malimi Busungu na Mateo Anthony.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic