December 18, 2015


Kuelekea mchezo wa Yanga dhidi ya Stand United, mshambuliaji na kinara wa mabao wa Stand, Elias Maguri, amefunguka kuwa hana hofu na mabeki wa Yanga kwa kuwa anawafahamu vizuri na kudai kuwa atapambana kusaidia kuibeba timu yake ingawa anajua upinzani utakuwa mkubwa.

"Bossou simjui, Yondani si mgeni kwangu, si watu ambao wanaweza kunipa shida. Kwa kushirikiana na wenzangu najua tutapenya na kufanya vizuri," alisema.

Yanga wenye alama 27, watavaana na Stand yenye pointi 19, kesho Jumamosi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, ambapo Yanga ilishinda mechi iliyopita dhidi ya African Sports huku Stand ikipata kipigo kutoka kwa Mwadui FC.


Kwa upande wa Yanga, safu ya ulinzi imekuwa ikiongozwa na Kelvin Yondani, Juma Abdul, Haji Mwinyi na Vincent Bossou ambaye amechukua nafasi ya Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye ni majeruhi.

Hata hivyo, Stand United nayo imekuwa ikipoteza mwelekeo kutokana na kwenda kwa kusuasua katika mechi zake.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic