December 26, 2015


Yanga leo inacheza na Mbeya City katika Ligi Kuu Bara bila nahodha wao, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, lakini Kocha Hans van Der Pluijm amesema hakuna shida yupo Vincent Bossou.

Pluijm amepanga kumtumia Bossou raia wa Togo kucheza nafasi ya Cannavaro ambaye anaguza jeraha la kisigino cha mguu wa kulia ambalo litamuweka nje kwa wiki tatu.

Cannavaro tayari ameukosa mchezo dhidi ya Stand United ambao Yanga ilishinda mabao 4-0 na ule dhidi ya African Sports jijini Tanga ambapo Jangwani ilsihinda bao 1-0. 

Pluijm amewatoa hofu wanachama na mashabiki wa Yanga, kuhusu pengo la nahodha huyo kwamba Bossou yupo kwa ajili hiyo na kwamba wala wasiwe na shaka.

Mdachi huyo alikwenda mbali kwamba bado ana matumaini kibao na pacha ya Bossou na Kelvin Yondani ambayo kwa mara ya kwanza haikupitisha bao katika katika mchezo uliopita.

“Mara zote kanuni zangu zipo wazi, huwa siangalii nani hayupo kikosini, badala yake naangalia jinsi ya suluhu ya ukosefu wa mchezaji. Kweli tutamkosa Cannavaro kwa wiki tatu hivi kutokana na vipimo kuonyesha ana kasoro kwenye kisigino, atakuwa nje kwa wiki tatu lakini siwezi kuzungumzia pengo lake.


“Mara zote napenda kuweka akili kwa kikosi nilichonacho. Hayupo (Cannavaro), Bossou yupo kwa ajili hiyo, nafurahi ameanza vizuri na Yondani, hawakuruhusu bao, sasa nawezaje pengo la Cannavaro?” alihoji kocha huyo wa zamani wa Chelsea Berekum.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic