Kutokana na ujio wa straika, Paul Kiongera ndani ya kikosi cha Simba umeonekana kumchanganya kocha wa timu hiyo, Dylan Kerr kutokana na kusema hajui ni wapi ataweza kumpachika straika huyo kwenye mfumo wake kiasi cha kuanza kufikiria kubadili mfumo wake ili straika huyo acheze.
Kerr ambaye timu yake itacheza na Azam FC kesho Jumamosi, alisema tangu Mkenya huyo atue, amekuwa akitafuta mbinu mpya ya kumfanya apate nafasi ya kucheza.
“Nafikiria jinsi ya kumuanzisha kwenye kikosi cha kwanza kwa sababu sasa hivi tuna rundo la washambuliaji ambapo hao wote wana viwango vya hali ya juu huku kila mmoja akijaribu kupambana kwa uwezo wake ili kupata namba,” alisema Kerr.
Kwa sasa Simba ina mafowadi watano wakiwemo Hamis Kiiza, Mussa Mgosi, Daniel Lyanga, Ibrahim Ajib pamoja na Kiongera.








0 COMMENTS:
Post a Comment