December 11, 2015


Mshambuliaji Papa Niang raia wa Senegal amesema iko siku atarejea nchini na kucheza soka.


Kwa sasa kw amujibu wa yeye Niang yuko nchini Finland anakipiga katika kikosi cha FF Jaro.

Niang alitua nchini Agosti 21, mwaka huu na kukaa nchini kwa siku nne pekee, kwani Simba ilipomaliza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mwadui FC uliopigwa Agosti 24, ikatangaza kuachana naye, kesho yake akaondoka.

Straika huyo alionekana si kitu kwa Simba kutokana na kutokuwa fiti licha ya mwenyewe kukiri kwamba awali aliwaambia viongozi wa Simba kuhusu hali yake hiyo, lakini walimlazimisha kuja kufanya majaribio hivyohivyo.

Akizungumza kutoka Finland, Niang alisema: “Baada ya Simba kuniacha, nikarudi katika timu yangu ya zamani ya FF Jaro huku Finland. Nimecheza soka miaka nane hapa, sasa nahitaji changamoto mpya ya kwenda kucheza soka nje ya nchi hii.

“Nilifurahi Simba iliponipa mwaliko wa kufanya majaribio lakini bado sijakata tamaa, ipo siku nitarudi tena huko lakini siyo tena kujiunga na Simba, nataka kuichezea timu nyingine ili niwaonyeshe Simba kwamba walikosea kunitimua haraka.

“Nimeshaongea na wakala wangu, Regis ambaye ni Mcameroon, ananifanyia mipango hiyo lakini kinachokwamisha ni kukosa mawasiliano ya karibu na timu nyingine zaidi ya Simba.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic