December 25, 2015


Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr amesema mshambuliaji, Ibrahim Ajib atakuwa msaada mkubwa katika kikosi chake zaidi ya sasa.

Hata hivyo amesema mshambuliaji huyo kinda anahitaji kujituma zaidi ili kuhakikisha kipaji chake kinapanda.

"Kipaji lazima ukilinde, lazima ukiendeleze pia. Ajib ni mchezaji mzuri sana, sasa ni msaada lakini anaweza kuwa msaada zaidi," alisema.

Kocha huyo pia amesifia kipaji cha mchezaji huyo ambaye amekuwa akiwa katika 'mudy' anafunga mabao muhimu na mengi.

Hata hivyo, Ajib naye amekuwa ni mshambuliaji "anayelala na kuamka". Kwani anaweza kufunga bao halafu akakaa baada ya miezi rundo bila ya kufunga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic