Yanga ambao ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara imepanga kuingia kambini leo Jumatano kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City, kwenye Uwanja wa Taifa Dar, Jumamosi hii.
Watoto hao wa Jangwani wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Stand United kwenye mchezo uliopita.
Kocha wa Yanga, Mholanzi Hans van Der Pluijm, amesema wameamua kuingia kambini ili waweze kujiandaa vyema na mchezo huo ambao anautazamia kuwa ni mgumu lakini akagoma kuweka wazi sehemu watakapoiweka kambi hiyo.
“Yah, tutaingia kambini Jumatano (leo) kwa siku chache kwa ajili ya kujiwinda, mechi ya Mbeya City si nyepesi tutahitaji kujipanga zaidi kama kweli tunataka kuendelea kupigania kukaa kileleni na kufanikiwa tulipokusudia mwisho wa msimu huu,” alisema Pluijm.
Hata hivyo, chanzo makini kutoka ndani ya timu hiyo kimeeleza kuwa kambi hiyo imepangwa kuwekwa katikati ya jiji karibu na makao makuu ya klabu hiyo na hii ni kutokana na mchezo huo kupigwa Dar hivyo wanataka kubaki hapahapa karibu.







0 COMMENTS:
Post a Comment