December 23, 2015


Yanga italazimika kufanya maamuzi magumu. Aidha ikubali kumpoteza kiungo wake, Sina Jerome, ama ikubali kumtunza, ale, kulala na kuishi bure na kusubiria dirisha kubwa la usajili msimu ujao, kwani taarifa za kuaminika uwezekano wa kumsajili kipindi hiki ni mgumu sana.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Yanga ilimshusha kiungo huyo mshambuliaji raia wa Rwanda kwa ajili ya majaribio lakini ghafla amewakuna viongozi na wanachama wa klabu hiyo wanaohudhuria mazoezi ya kikosi hicho kwenye Uwanja wa Boko Veterani, Ununio kutokana na uwezo wake wa mashuti, pasi za rula na manjonjo ya kuchezea mpira.

Yanga ilitaka kumsajili kwa ajili ya kumtumia kwenye michuano ya kimataifa (Caf) baada ya dirisha la usajili Bongo kufungwa tangu Desemba 15, mwaka huu kwani usajili wa Caf wenyewe utafungwa Desemba 31, mwaka huu, hivyo kuipa nafasi timu yoyote inayoshiriki kimataifa kuendelea na usajili.
Lakini kikwazo kikubwa kilichoelezwa ni kwamba Caf haiwezi kwenda kinyume na sheria za wanachama wake ikiwemo TFF.

“Jerome kweli ni mzuri, sema huenda tukamkosa hivihivi. Ujue pamoja na dirisha la Caf kuendelea lakini kumbuka sisi tumejaza nafasi zote saba za wachezaji wa kigeni wanaotakiwa na TFF na wao Caf wanafuata sheria za wanachama wao, hivyo hawawezi kupokea majina ya wachezaji nane badala ya saba wanaotambulika TFF,” kilisema chanzo chetu na kuendelea.

“Angalau ingekuwa usajili wa TFF umefungwa halafu tukawa na nafasi ya ziada, tungemsajili kwa ajili ya kimataifa. Yaani dah..! Sijui tutafanyaje lakini naona kwa vyovyote vile tunamtunza. Hakuna aliye tayari kumpoteza.”

Alipotafutwa katibu wa Yanga kulitolea ufafanuzi, kama kawaida yake simu yake haikupokelewa.

Lakini kwa upande wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa Ofisa Habari wake, Baraka Kizuguto, lilisema kuwa Yanga hawawezi kumtumia mchezaji huyo kwa kuwa ni lazima awe na leseni ya ligi ya ndani.


“Yanga hawawezi kumtumia mchezaji huyo kwa kuwa anatakiwa kuwa na leseni ya usajili wa ligi ya ndani.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic