December 18, 2015

SINA MAZOEZINI YANGA LEO
Kiungo wa Rayon Sports, Jerome Sina ametua Yanga na kufanya majaribio.

Jerome ni sehemu ya usajili inaotarajia kuufanya Yanga kwa ajili ya michuano ya kimataifa.

Bado haijajulikana atafanya majaribio ya muda gani lakini Kocha Hans van der Pluijm amesema bado wanamuangalia.

“Anaangaliwa na tunahitaji muda kidogo, tutawaambia nini kinachofuata,” alisema katika mazoezi ya Yanga kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam, leo.


Jerome aliwahi kukipiga Rayon Sports lakini taarifa zinaeleza kuwa ni mmoja wa viungo bora kiuchezaji uwanjani ingawa ni mtukutu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic