Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr raia wa Uingereza amesema mechi yao dhidi Toto African kesho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza itakuwa ngumu lakini wanachotaka ni pointi tatu.
Kerr amesema ameelezwa historia ya ugumu wa mechi dhidi ya Toto, lakini kwa kuwa wanataka pointi tatu, kila kitu watakiacha nyuma.
"Pointi tatu ndiyo jambo muhimu sana, ushindani ni sehemu ya ligi. Tutaacha mambo mengine yote ya historia nyuma na kuangalia tunachotaka ambacho ni pointi tatu.
"Tunajua mechi ya mwisho wameshinda mabao matano ugenini, hilo linakuwa ni sehemu ya maandalizi yetu kabla ya kukutana nao," alisema.
Katika mechi yake ya mwisho, Toto African iliishindilia Majimaji kwa mabao 5-1 ikiwa nyumbani kwao Songea huku Simba ikionyesha kiwango kizuri lakini ikaambulia sare ya mabao 2-2 dhidi ya Azam FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment