Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima atazungumza na wanachama na mashabiki wa Yanga jijini Dar es Salaam, leo.
Niyonzima anatarajia kufanya hivyo katika mkutano wa waandishi wa habari uliopangwa kufanyika jijini Dar.
Mpashaji mmoja amesema huenda Niyonzima akafanya mkutano huo makao makuu ya klabu ya Yanga.
"Sina uhakika sana, lakini mkutano huo unaweza kufanyika palepale klabuni na Niyonzima ndiye atakuwa mzungumzaji mkuu," alitoa taarifa hiyo, mpashaji.
Taarifa zinaeleza, Niyonzima ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda ameamua kufanya hivyo kwa lengo la kumaliza mgogoro.
Hadi sasa, klabu ya Yanga imeishatangaza kuvunja mkataba na Niyonzima kwa madai ya utovu wa nidhamu.
Lakini taarifa zinaeleza, hadi sasa bado uongozi wa Yanga haujampa barua ya kuvunja mkataba huo hadi sasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment