Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima amewaomba mashabiki, wanachama na viongozi wa klabu hiyo kongwe nchini kumsamehe.
Niyonzima raia wa Rwanda amewambia kama aliwakosea, anaowamba wamwie radhi.
“Kama mtoto akikosea lazima arudi na kuoma msamaha, ninaomba radhi kama niliwakwaza kwa kila kilichotokea,” alisema Niyonzima.
Akizungumza kwenye makao makuu ya klabu ya Yanga mtaa wa Jangwani na Twiga jijini Dar es Salaam, kiungo huyo wa zamani wa APR ya Rwanda alisisitiza kwamba ataendelea kuitumikia klabu yake kwa juhudi zote.
"Bado nina kiu ya kuitumikia Yanga kwa juhudi zote, najua mimi ni sehemu ya Yanga, ninatamani kurudi na kushirikiana na wenzangu kuendelea kupambana kwa ajili ya Yanga.

Tayari klabu ya Yanga imeishatangaza kuvunja mkataba na Niyonzima kwa madai ya utovu wa nidhamu.
Hata hivyo, hadi leo anaomba radhi, uongozi wa Yanga haukuwa umemkabidhi barua rasmi ya kuvunja mkataba.
Inapendeza,mchezaji unaependwa na mashabiki hivyo kuomba msamaha.
ReplyDeleteYanga msiremberembe kwenye maamuzi.Safi sana Niyonzima.