January 8, 2016


Kocha Herve Renard wa Ivory Coast ameteuliwa kuwa Kocha Bora barani Afrika. Kocha huyo ameshinda tuzo hiyo katika tamasha la kuwatuza wachezaji bora wa Afrika linaloendelea hivi punde jijini Abuja, Nigeria.

Renard raia wa  Ufaransa ameteuliwa kuwa kocha bora kutokana na mafanikio yake kwa mwaka 2015. Mpinzani mkubwa kwake alionekana ni Patrice Carteron, hata hivyo hakufua dafu.


Kocha huyo ameiwezesha Ivory Coast kubeba ubingwa wa Afrika ikiwa ni mara yake ya pili kufanya hivyo baada ya miaka michache kuwa ameiwezesha Zambia kubeba ubingwa wa Afrika.

Lakini Novemba 11, mwaka jana kocha huyo alitimuliwa kazi Lille ya Ufaransa baada ya kuingoza timu hiyo kucheza mechi 13, ikaambulia pointi 13 tu.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic