FARID |
Na Saleh Ally
ULIONA wakati Watanzania walivyokuwa na furaha kubwa baada ya kupata taarifa mshambuliaji nyota wa TP Mazembe, Mbwana Ally Samatta sasa anaanza safari ya kwenda Ulaya?
Samatta ameamua kuanza safari ya kwenda Ulaya akiwa na rekodi ambayo watu wengi hawakuwa wakiizungumza, badala yake waliangalia ile tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika wa ndani.
Rekodi hiyo ni kwamba, Samatta anakwenda Ulaya akiwa mchezaji wa kwanza anayekwenda kucheza soka barani Ulaya akiwa amenunuliwa na hakuna majaribio.
Hakuna mchezaji wa Tanzania ambaye ametoka nchini kwenda kucheza Ulaya akiwa ananunuliwa na kwenda kucheza na si kufanyiwa majaribio ili kuangalia ubora wake.
Pia hii ni rekodi kwa Bara la Afrika pia, kwamba wachezaji wengi hata kutoka Nigeria, Cameroon, Liberia, Misri na kwingine, wamekuwa wakifanyiwa majaribio ili kuangalia ubora wao.
SIMBA |
Samatta anakwenda moja kwa moja, tena akiwa anagombewa na klabu mbalimbali. Huenda ni jambo zuri na changamoto kubwa kwa wachezaji wengine wa Tanzania. Ifikie nao wanunuliwe moja kwa moja, tena wawe wanachagua klabu ipi wanayotaka kwenda.
Wakati furaha ya Samatta kwenda Ulaya ikiwa inapamba moto wakati huo, kikubwa ambacho kinaweza kuwa gumzo na kikwazo kwa wachezaji wetu ni suala la umri.
Kwa mujibu wa rekodi za Samatta anakwenda Ulaya akiwa na miaka 24, niseme ni jambo zuri kama kila kitu kipo sahihi. Hata kama Samatta atakuwa amechelewa kidogo, lakini akifanya vizuri bado atakuwa na uhai wa soka barani humo.
Ambacho nalenga kukizungumzia ni kuwaasa wachezaji wengine wa hapa nyumbani kuhusiana na suala la umri, hasa suala la kudanganya. Lazima tukubali wachezaji wa Kiafrika wamekuwa wakiongoza kwa kudanganya kuhusiana na umri wao.
Hakuna ambaye amewahi kuongeza umri wake, lakini wamekuwa wakipunguza ili kuonekana vijana zaidi na nchi za Afrika Magharibi zinaongoza katika hilo na Ulaya wanalijua na wamekuwa wakilalamika sana.
Kwa kuwa kipindi hiki Watanzania wengi sasa wameonekana kuhamasika baada ya kuona Samatta anakwenda Ulaya, basi lazima wapige hesabu ya umri ili kuepusha suala la umri kuwa kikwazo kwao.
Ninaamini umesikia sakata la Klabu ya AC Milan ya Italia kuamua kumfikisha kizimbani mchezaji wake wa zamani Yusupha Yaffa, raia wa Gambia ambaye alidanganya umri wake kwamba ana miaka 19 kumbe ana 28.
Milan imeamua kumfikisha mahakamani kabisa mshambuliaji huyo ambaye sasa anakipiga katika kikosi cha MSC Duisburg cha nchini Ujerumani.
Mgambia huyo alichokifanya si kigeni, utagundua wachezaji wengi wa Kiafrika wanakosea hesabu za kuanza kuangalia kwenda Ulaya kwa kuwa hawakubali kuondoka mapema nyumbani kwao.
TOTO AFRICAN |
Angalau wanataka kula matunda na kuona wakishangiliwa na kutukuzwa, mfano kwa hapa, Yanga na Simba ndiyo mwisho wa reli kwao.
Tunajua kuna wachezaji wamekuwa wakikataa kwenda Ulaya kutokana na sifa wanazopata kwa mashabiki, furaha wakitembea barabarani wanachukuliwa utafikiri waheshimiwa.
Baada ya kufikisha miaka 25 au 27, ndiyo wanaanza kufikiria kwenda Ulaya na wakati huo wanakuwa wamechelewa, mwisho itakuwa ni kukimbilia kupunguza umri au kutumia ule unaojulikana hivi “umri wa passport”.
Umri wa passport ni furaha kama mchezaji hatagundulika, lakini ikitokea mambo yamekwenda hovyo, basi ni kulichafua jina la nchi husika, pia klabu aliyotokea na Wazungu wanakuwa wepesi kukasirishwa na uongo hasa katika masuala ya msingi, kama umri.
Wachezaji ambao wamefikisha miaka 25, vizuri wakasahau kabisa suala la Ulaya ili kuepuka kuingia kwenye hisia za kutaka kuficha.
FRIENDS OF SIMBA |
Pia ni vizuri zaidi kwenda Ulaya mchezaji akiwa na miaka chini ya 20, angalau Farid Mussa wa Azam FC ambaye anakwenda Slovenia kufanya majaribio. Akipasi, akaanza kucheza akiwa na umri huo, atakuwa na nafasi ya kupambana na ndani ya miaka minne akawa amefika Ufaransa, Italia, Hispania au England, tena akiwa na makuzi ya soka ya Kiulaya.
Akipata nafasi katika timu nyingine, hatasumbuka sana kwa kuwa tayari amezoea mazingira ya Ulaya. Hivyo kujipima mapema ni vizuri.
Msisitizo ni hivi, Wazungu wanazidi kuinua macho na wakali zaidi kuhusiana na suala la umri kama yaliyomkuta Mgambia huyo anayeumbuka na kuingia kwenye msukosuko mkubwa ambao utamfanya amalize maisha yake ya soka na migogoro badala ya kukaa na kufurahia. Ninawaonyesha, kuweni makini sana.
Umesema kweli kabisa.Kuficha umri ni funza anaesumbua mastaa wengi hapa Tanzania kwa ujumla.Ni wachache sana husema ukweli ana umri gani,wengi husherehekea siku zao za kuzaliwa lakini ukimuuliza una umri gani wanakuwa na kigugumizi kutaja umri,huwa sijui kwa nini.
ReplyDelete