January 17, 2016

HII LEO

Gazeti la Tanzania Daima kitengo cha michezo limeendelea kula raha na picha zinazochapishwa katika blogu ya Salehjembe huku likijisifia kutumia waandishi wake.

Tanzania Daima limekuwa likifanya hivyo kwa kuchukua picha zinazochapigwa na blogu hii, linafuta nembo na baadaye kuandika hivi PICHA NA MWANDISHI WETU.

Mfano mzuri ni ule wa picha ya Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ikionyesha anauza duka. Wenyewe wakaichapisha siku iliyofuata na kuandika na MPIGAPICHA WETU.

Mara kadhaa, SALEHJEMBE imefikisha malalamiko hayo kwamba si sawa na iko tayari kuona gazeti hilo halitumii picha zake kama inashindwa kuonyesha kuthamini kazi ya blog hii.

Angalau kungekuwa hakuna nembo, wanaiona nembo na kuifuta halafu wanaandika picha ya mpigapicha wao wakati wakijua kabisa hakuna mpigapicha wa SALEHJEMBE anayefanya kazi Tanzania Daima.

Juhudi za kuzungumza na wahariri wake wa michezo akiwemo Tullo Chambo zimefanyika zaidi ya mara moja, lakini suala hilo linaonekana kuendelea kwa kasi bila ya haya hata kidogo.

Mwandishi mwingine wa Tanzania Daima, Salum Mkandemba aliwahi kuahidi hilo halitajirudia, lakini anaonekana kushindwa kuzuia “dezo dezo” hiyo inayoendelea huku ikilazimisha Salehjembe ni mpigapicha wa gazeti hilo, kitu ambacho ni uongo wa wazi na usiovumilika hata kidogo.

USHAURI:
Kwao Tanzania Daima kitengo cha michezo, kama wanavutiwa na picha za blogu hii, wanaruhusiwa kutumia lakini waonyeshe wamezitoa wapi kwa maandishi au waache nembo ya SALEHJEMBE.COM ikielea kama ilivyo.

Wakishindwa, chaguo ni lao, waache kutumia kabisa ili kuonyesha wana uwezo wa kupata wanachotaka bila ya kuandika uongo kuwa SALEHJEMBE ni mpigapicha wa gazeti hilo.




1 COMMENTS:

  1. Nazani unatakiwa kuwashitaki hata ikibidi kudai fidia. Si sahihi kuchapisha bila ridhaa au kutambulisha chanzo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic