Hiki ndicho kikosi cha kwanza cha Yanga ambacho kimepoteza mechi ya Ligi Kuu Bara msimu huu.
Lakini ndiyo kikosi cha kwanza cha Yanga kupoteza mchezo wa mashindano ndani ya dakika 90 na ndani ya wachezaji 11, kilikuwa na wageni watano.
Wageni hao ni Amissi Tambwe (Burundi), Vicent Bossou (Togo), Mbuyu Twite (Rwanda), Donald Ngoma na Thabani Kamusoko (Zimbabwe).
Baadaye aliingia Boubacar Gaba raia wa Niger ambaye pia hakuweza kutoa msaada wa kubadilika matokeo Coastal Union kushinda kwa mabao 2-0.
Ndani yake, washambuliaji hatari, Tambwe mwenye mabao 13 kileleni na Ngoma mwenye 9, pia walishindwa kuikoa Yanga.
Hiyo ni sehemu tosha ya kuonyesha, soka ni mchezo usiobashirika kilahisi. Umekuwa ukipendwa zaidi kutokana na matokeo yake na mechi ya Coastal Union na Yanga, ni mfano.
0 COMMENTS:
Post a Comment