Yanga imeitwanga Mtibwa Sugar kwa mabao 2-1 na kukaa kileleni Kundi B katika michuano ya Mapinduzi.
Kwa ushindi huo, Yanga imefikisha pointi sasa inasubiri mshindi wa pili kundi A lenye timu za Simba, JKU, URA na Jamhuri.
Katika mechi ya leo, Mtibwa Sugar ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Shiza Kichuya katika dakika ya 10 kabla ya Yanga kusawazisha kupiitia Issoufou Boubacar katika dakika ya 42.
Boubacar alifunga bao safi la mkwaju wa adhabu, pembeni kabisa na kuamsha shamrashamra kwa mashabiki wa Yanga waliojitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
YANGA |
Timu hizo zilikwenda mapumziko kwa sare ya 1-1 na baada ya hapo ilikuwa ni kushambuliana kwa zamu huku Yanga ikionekaan kuimarika zaidi baada ya kuwaingiza Salum Telela, Malimi Busungu na Paul Nonga.
MTIBWA |
Yanga ilipata bao la pili kupitia Malimi Busungu katika dakika ya 82 akiunganisha krosi safi ya Simon Msuva na mabeki wa Mtibw Sugar wakamsahau hivyo kupata nafasi ya kupiga kichwa akiwa peke yake na mpira ukamshida kipa Said Mohammed Mduda.
Mkongwe Henry Joseph aliyeingia, alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya kiungo Telela.
0 COMMENTS:
Post a Comment