February 26, 2016


Kikosi cha Coastal Union wameonyesha wanaweza baada ya kuitwanga Mtibwa Sugar kwa bao 1-0 na kuing'oa katika Kombe la Shirikisho linalodhaminiwa na Azam Sports HD.

Wachezaji wa Coastal Union jana walitangaza mgomo hadi wapewe fedha zao za mishahara ya miezi mitatu. Lakini leo saa moja kabla ya kwenda uwanjani, wakalipwa mshahara wa mwezi mmoja kila mmoja.

Hali iliyowafanya waingie kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kuhakikisha wanaimaliza Mtibwa Sugar.

Imeelezwa uongozi umewaahidi kumalizana nao baada ya mechi ya leo.

Wachezaji hao pia walilalamika kuhusiana na mazingira wanayoishi kutokuwa mazuri na kuutaka uongozi kuyaboresha huku baadhi wakimuomba aliyewahi kuwa madhamini wa Coastal Union, Nassor Bin Slum, kurejea kuokoa jahazi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic