February 16, 2016


Baada ya kumaliza majukumu ya kimataifa kwa ushindi wa bao 1-0 nchini Mauritius, Yanga sasa akili na nguvu zote ni Jumamosi.

Yanga imetua salama mjini Pemba na kuanza kambi na Kocha Hans van der Pluijm, amesema wanachoangalia kwa kila jicho ni Jumamosi.

“Kila kitu kinaenda vizuri na matarajio ni upinzani mkali. Hivyo acha tuendelee na maandalizi,” alisema.
Pluijm hakutaka kuzungumza zaidi na badala yake akasema maandalizi ya Pemba ni sehemu ya maandalizi tokea mwanzoni mwa msimu.


“Ni kipindi cha presha, hivyo acha tufanye kazi,” alisisitiza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic