Kikosi cha Simba chini ya Jackson Mayanja, kinaongoza kwa mabao 2-0 hadi wakati wa mapumziko katika mechi ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports HD kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Bao la kwanza la Simba lilipatikana katika dakika ya 3, mfungaji akiwa ni Danny Lyanga aliyeunganisha krosi ya Emiry Nimubona.
Dakika ya 19, Hamisi Kiiza naye akafunga bao la pili akimchambua kipa baada ya kuvunja mtego wa kuotea.
Baada ya hapo, Simba waliendelea kuutawala mchezo kwa kiasi kikubwa huku wakipoteza rundo la nafasi za kufunga.
Kiiza, Lyanga, Brian Majwega, Mwinyi Kazimoto na Jonas Mkude ndiyo waliopoteza nafasi hizo wakiwa katika nafasi nzuri kabisa ya kufunga.
Simba ilikuwa na nafasi ya kuibuka na mabao hata matano katika kipindi cha kwanza pekee.
0 COMMENTS:
Post a Comment