Wakazi wa jiji la Mbeya kesho watakuwa na kazi moja tu, pambano la watani na wapinzani wakubwa katika mchezo wa soka, Mbeya City wanakutana na Prisons.
Timu hizo safari hii zinakutana katika Kombe la Shirikisho la Azam Sports HD ambalo sasa limeanza kupata kasi kimsisimko.
Mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports HD litapigwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Tayari joto lake ni kubwa na majigambo kutoka kila sehemu yakiongezeka na hii inatokana na kwamba, katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu Bara, timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana. Sasa kazi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment