September 15, 2021

 


IMEELEZWA kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia amepewa mechi mbili ikiwa ataboronga safari itamkuta.

Nabi kibarua chake kimeanza kuwa katika wakati mgumu baada ya kushindwa kufanya vizuri katika mechi mbili za hivi karibuni baada ya Ligi Kuu Bara kumeguka kwa msimu wa 2020/21 na sasa ni muda wa maandalizi ya msimu mpya.


Ilikuwa ni ile ya Wiki ya Mwananchi ambapo ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 1-2 Zanaco siku hii ilikuwa ni rasmi ya utambulisho wa kikosi kazi cha Yanga kwa msimu wa 2021/22.

Pia mchezo wa pili ilikuwa ni ule wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali ambapo Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 0-1 Rivers United.

Awali Nabi aliweka wazi kuwa anahitaji muda ili kukiimarisha kikosi hicho kwa kuwa hakupata muda mzuri wa kuwaunganisha wachezaji wake kutokana na kambi ya Morocco kutokuwa kwenye  mpangilio mzuri.

Mechi ambazo inaelezwa kuwa amepewa ni ile ya marudio itakayochezwa nchini Nigeria pamoja na ile ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, Uwanja wa Mkapa Septemba 25.


13 COMMENTS:

  1. Replies
    1. Mwandishi uchwara. Anaandika habari ambayo haina uhalisia. Anataka kuuza gazeti kisa vyuma vimebana?

      Delete
    2. Kwakweli namuonea ghuruma Sana Kocha Nabi ni kocha wa mpira ila ameingia kwenye chaka la wanamihemko. Ireal feel sorry for him. He is in a wrong spot.

      Delete
  2. Acheni kuweweseka nyie utopolo bado mapema

    ReplyDelete
  3. Mbona mwanaspoti wakiwasifia kuliko maelezo hamlalamiki?Mnajazwa ujinga bila uhalisia.

    ReplyDelete
  4. Huyo keshakalia kuti kavu na atangolewa kama jino bovu. Na yule mwengine aroweke nywele kwa sabuni kupunguza ukali wa uwembe

    ReplyDelete
  5. Kila watavo mtisha ndipo atapozidi kuvuruga. Yeye keshaahidi kuwa huu ni mwaka wa makombe

    ReplyDelete
  6. Nabi haendi kokote hata muombee vipi!

    ReplyDelete
  7. Mamabo yakizidi kumuelemea yeye mwenyewe atabwaga manyanga kwa kujiondoa kabla ya kumfika aibu ya kutimuliwa

    ReplyDelete
  8. Kocha mbona yupo vzr, kuna baadhi ya viongozi wanaingilia mambo ya kocha, sasa basi endapo watamtoa huyu kocha basi wataharibu kila kitu, bora tuvumilie tuone ligi inaanzaje.

    ReplyDelete
  9. Halafu we andika kuwa Simba wajiendae kwa maisha mapya bila Hans Pope,wengi tunajua mkono wake kwenye soka fitna alikuwa kinara au Mkuu wa Kikosi .

    ReplyDelete
  10. Hanspope pengo ndani ya simba alikuwa moja kati ya wasaidizi mahiri wa Mo sio siri ila ametuachia Misingi imara ya kimawazo na vitendo jinsi gani ya kuipigania klabu.

    ReplyDelete
  11. Nyie waandishi wa habari wajinga wajinga iv hamnaga cha kuandika nani aliyempa nabi mechi 2 acheni kuzuazua msivyovijua mmetumwa nini acheni ujinga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic