MAMIA ya mashabiki wa Yanga, Agosti 27 walijikuta wakishinda mchana kutwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam kumpokea mshambuliaji wao mpya, Yacouba Sogne ambaye ilishindikana kutua nchini.
Awali, Yanga kwa kupitia Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli alitoa taarifa za kuwasili kwa mshambuliaji huyo saa 7:20 mchana kwa ndege aina ya Ethiopia Airline akitokea Burkina Fasso.
Mshambuliaji huyo ni kati ya wachezaji waliosajiliwa na timu hiyo katika kuelekea msimu mpya wa 2020/2021 akitokea Asante Kotoko ya Ghana.
Mashabiki hao walianza kufika kwenye uwanja huo wa ndege kuanzia saa nne asubuhi baadhi wakiwa wamevalia jezi zao zenye rangi kijani na njano zenye chapa ya Kampuni ya GSM.
Kundi hilo la mashabiki walionekana kujazana kwenye mlango mkubwa wa kutokea abiria uliokuwepo uwanjani hapo huku wengine wakiwa wamekaa kwenye maegesho ya magari.
Mamia hayo ya mashabiki baadhi walionekana kufika uwanjani hapo na magari yao ya kukodi aina ya Toyota Coaster huku wengine wakiwa na magari madogo ya binafsi, bodaboda.
Mashabiki hao walionekana kuanza kutawanyika mara baada ya kauli ya Muhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz kutoa taarifa za mshambuliaji kutua leo kupitia mtandao wa Instagram.
“Mshambuliaji wetu Yacouba hatakuja tena leo (jana) na badala yake atakuja kesho (leo), hivyo niwatake mashabiki wa Yanga kufuatilia taarifa mbalimbali kupitia mitandao yetu ya kijamii,” alisema Nugaz.
Taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo alikwama nchini Burkina Faso na anatarajiwa kuanza safari kesho ya kuja Bongo.








Wanaacha kazi zao Wanakwenda kushinda kutwa eyapot halafu wanarejea. Wanatia huruma
ReplyDeleteMwandishi, acha propaganda zako za kutaka kututoa kwenye njia! Tuache tukamilishe kilele cha wiki ya wananchi wakati wewe ukiendelea na mambo ya timu yako. Tuache wananchi tuna jambo letu mwaka huu
ReplyDeleteHuna hbr za kuandika leo siku ya tatu tushazichoka ndo unazileta ila umekosa sifa kabisa maana siku hz unaandika pumba tupu
ReplyDeleteHuyu mwandishi upeo wake wa kufikiri mdogo sana!!
Deletesio lazima mke wako uliyemuoa wewe awe chaguo pendwa kwa wanajamii na ndugu zako wote, na ajabu sasa ni kwamba huwezi sema kwamba uachane nae hivyo unapokuta taarifa chapishwa yoyote katika salehejembeblogsport.com haikuvutii ama haikuhusu wewe pita kushoto na unaachana nayo ili wasome wanayoiona na kuidhania kwamba yaweza ikawa story nzuri na yenye kuvutia kwao.
ReplyDeleteAcha shobo wewe! Kichwa cha habari ni tofauti kabisa na habari yenyewe ukiachilia mbali kukosekana kwa uwiano.
DeleteHaikubainishwa popote ambapo mshambuliaji alitoa taarifa ya kufika kwake saa 7 halafu akakosa kufika; kawasoteshaje?!
Kwani inapochapishwa taarifa si lazima I we na Ukweli ndani yake?.Lakini taarifa Kama inapotosha si lazima watu wahoji na Kama sikosei hii blog mmiliki wake ana leseni na amepewa kutoa habari au taarifa zilizo sahihi.Bahati kwenye mpira hapana TCRA ni shamba la Bibi, Waandishi wamebaki na TCRA yao mahaba kwa baadhi ya Club, habari Za mikia humu always za kutia matumaini za kujenga nk ,cse mnajuana.USIPINGE.Ukisoma Bwalya chanya,MuAngola tofauti hapo wamewekwa headline wote.Kwani hii blog imewekwa nani wasome MO?ndo Maana akasema Mwananchi/Mwanaspoti nawatafuta japo Ni zimwi likujualo lkn mliishia kucheka tu
ReplyDeleteMIKIA FC ASILIMIA 90 WANAULEMAVU WA AKILI.
ReplyDeleteMiyanga inachefua kweli kosa likowapi hapo?kichwa habari kinaendana kabisa na habari yenyewe.Walisota bila mafanikio kwani alikuja?achani kumshambulia mwandishi.Rudini darasani mkajifunze kutafuta vichwa vya habari
ReplyDelete