Mshambuliaji Mbwana Samatta ameanza kuonyesha cheche zake barani Ulaya baada ya kuisaidia Genk kupata ushindi wa mabao 3-2 katika mechi ya Ligi Kuu ya Ubelgiji.
Samatta amefunga bao la tatu wakati Genk iliyokuwa nyumbani ikiitwanga Club Brugge.
Wageni walianza kupata bao mapema katika dakikia ya 15 kupitia Thomas Meunier lakini Genk wasawazisha kwa mkwaju wa penalti wa Nikolaos Karelis katika dakika ya 36.
Thomas Buffel akaifungia Genk bao la pili katika dakika ya 50 lakini Hans Vanaken akajibu kwa kuifungia Club Brugge bao la pili.
Samatta ndiye aliyemaliza kazi zikiwa zimebaki dakika tisa mechi kwisha na kuihakikisha Genk pointi pointi tatu muhimu.
0 COMMENTS:
Post a Comment