February 8, 2016


Mshambuliaji nyota wa Simba, Mganda, Hamis Kiiza, ameiambia Yanga kuwa, kama wanataka waokote mipira mingi wavuni, basi wampange beki wa kati Mtogo, Vincent Bossou siku klabu hizo zitakapokutana Februari 20, mwaka huu.

Mtogo huyo, amekuwa akianza katika kikosi cha kwanza katika mechi za hivi karibuni mara baada ya Cannavaro kupata majeraha ya enka ambayo hivi sasa amepona na kuanza mazoezi mepesi kabla ya kujiunga na wenzake kwenye mazoezi ya pamoja.

Huenda Bossou akacheza mechi dhidi ya Simba kwa kuwa kuna uwezekano wa Kelvin Yondani kukosekana kutokana na kadi nyekundu aliyoipata katika kipigo dhidi ya Coastal Union wiki moja iliyopita.

Kiiza ambaye kabla ya mechi za jana alikuwa na mabao 14, alisema: “Kiukweli taarifa za kupona kwa Cannavaro zimenishtua, kwa maana yeye amepona, hivyo kurejea kwake huenda kukamtoa Bossou katika kikosi cha kwanza kwenye mechi dhidi yao.

“Mimi ninataka aanze kucheza Bossou ambaye ninaamini kwangu ni mwepesi kupitika, lakini siyo Cannavaro anayenipa tabu kumpita kila tunapokutana tangu nikiwa Yanga mazoezini.


“Ninajua Yondani katika mechi hiyo hatacheza kutokana na adhabu ya kadi nyekundu, huyo Bossou sijawahi kukutana naye lakini uwezo wake ninaujua vizuri, kama atacheza nina uhakika wa kufunga mabao mengi tu,” alisema Kiiza.   

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic