March 29, 2016

APR
Baada ya kupata mkikanda mitatu ya Yanga, Al Ahly imeanza kuifanyia kazi kupitia kocha wake, Martin Jol raia wa Uholanzi.

Lakini taarifa zinaeleza, mechi ya kwanza ambayo kocha huyo ameanza kuifanyia kazi ni ile Yanga iliyocheza mjini Kigali na kuifunga APR ya Rwanda kwa mabao 2-1.

YANGA

Kwa mujibu wa Mtanzania anateishi nchini Misri anaamini kocha huyo, lazima ataanza na mkanda huo kuiona Yanga inaposhiriki michyano ya kimataifa.

“Unajua wamepata mikanda mitatu, nimeambiwa mechi mbili ni Yanga akicheza mechi za Ligi Kuu Tanzania. Nafikiri kwa Jol lazima atataka wakati Yanga ikicheza mechi za kimataifa.

“Mechi dhidi ya APR inaweza ikawa msaada mkubwa kwa kocha huyo kwa kuwa atataka kuwajua Yanga wanachezaje wakiwa nje ya Tanzania na hasa katika michuano ya kimataifa,” alisema.

“Najua mfumo wao, kocha atasoma kila kitu halafu watakaa pamoja na kuchambua huku wakichangia nini cha kufanya,” alisisitiza Mtanzania huyo anayeishi nchini Misri kwa zaidi ya miaka 10 sasa.


Al Ahly itakuwa ya kwanza kusafiri ugenini, itaivaa Yanga Aprili 9 kabla ya mechi ya marudiano.

1 COMMENTS:

  1. Sio mbaya watawaona Tambwe na Ngoma ambao hawakuwa kwenye kiwango chao siku hiyo!!

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV